- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RIPOTI : TAKWIMU ZINAONESHA WAISLAMU 5,247 WAMEUAWA NA KIKUNDI CHA BOKO HARAMU KATIKA JIMBO LA ADAWAMA
Ripoti: Waislamu 5,247 wameuawa na Boko Haram katika jimbo la Adamawa
Baraza Kuu la Waislamu katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria limetangaza kuwa, kwa akali Waislamu 5,247 wameuawa na kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo hilo la kaskazini mwa nchi hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Gavana wa jimbo la Adamawa Alhaji Muhammadu Bindow amewaambia waandishi wa habari kwamba, zaidi ya Waislamu 5,100 pia wamejeruhiwa tangu mwaka 2013 kufuatia mashambulio tofauti ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo hilo.
Kiongozi huyo wa jimbo la Adamawa ametoa wito wa kusaidia wahanga wa mashambulio hayo ya Boko Haram na kujengwa na kukarabatiwa maeneo ya ibada pamoja na shule zilizobomolewa au kuharibiwa na mashambulio ya Boko Haram.
Aidha Alhaji Muhammadu Bindow ametaka kuimarishwa usalama na kupatiwa misaada vikundi vya jimbo hilo vilivyojitolea kupambana na wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kwamba, mbali na mauaji, mashambulio ya Boko Haram katika jimbo hilo yamesababisha hasara ya takribani dola milioni 220.
Mashambulizi ya Boko Haram yalianza mwaka 2009 nchini Nigeria kwa madai ya kupinga elimu zinazotoka nchi za Magharibi. Mashambulio ya genge hilo yalipanua wigo wake mwaka 2015 na kuingia pia katika nchi jirani na Nigeria, za Niger, Cameroon na Chad na hadi sasa zaidi ya watu 20,00 wanaripotiwa kuuawa kufuatia mashambulio hayo ya kigaidi ya wanamgambo wa Boko Haram.
Nchi nne za Cameroon, Nigeria, Chad na Niger zimeunda jeshi la pamoja la kupambana na magaidi hao lakini hadi sasa zimeshindwa kukabiliana vilivyo na mashambulio ya wanamgambo hao.