Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:46 am

PROF.TIBAIJUKA: WANANCHI TUKAE MKAO WA KUDADISI MAMBO

“Wananchi tukae mkao wa kudadisi mambo, ukiona mtu haeleweki humjui toa taarifa, ukiona kifurushi kimewekwa mahali usiwe mwepesi kuangalia nini usikute bomu limetegeshwa. Watu wabaya sana, wanataka kuharibu amani iliyopo kuivuruga,”amesema Prof. Tibaijuka

Kuhusu vijana hao wa jeshi la akiba, Prof. Tibaijuka amesema kuna mpango wa kufunguliwa kampuni ya ulinzi ili vijana hao wapate ajira sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama jimboni mwake hasa bomba la mafuta la Tanzania na Uganda linalotokea Tanga hadi Hoima nchini Uganda.

Vile vile ametoa fedha kwa ajili ya kununua sare za vijana hao walio maliza mafunzo jimboni kwake.

“Nilikua nawakumbusha miadi yetu kwamba tunakwenda kufungua kampuni ya ulinzi kusudi iwasaidie kupata ajira. Mimi kama mbunge wao lazima niwasaidie lakini huwezi pata ajira kabla ya kuweka miundombinu ya ajira.

Sasa ulinzi ni lazima, lazima uwe na vyombo vya ulinzi, ndio maana nakazana waunde kampuni, ulinzi umekuwa biashara ni fani inayopanuka sababu wahuni wamekuwa wengi, watekaji na kadhalika. Bomba letu la mafuta Rais John Magufuli amelileta na sisi angalau tuliunge mkono kwa kulilinda “amesema Prof. Tibaijuka.