- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
PICHA+10 MAPOKEZI YA RAIS WA KOREA KUSINI MJINI PYONGYANG KWA RAIS KIM
Pyongyang: Jana korea mbili zimeandika Historia nyingine baada ya Rais wa korea kusini Moon Jae- in kuzulu ikulu ya Rais Rais kim jong in na kujadiliana kuhusu kuondoa silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea na masuala mengine ambayo yamekuwa kiini cha mzozo baina yao.
Rais Moon Jae-in wa Korea kusini aliwasili Pyongyang kwa mkutano huo wa tatu kwa mwaka huu na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un.
Kabla ya kuanza kwa mkutano wao wa kilele rais wa korea kusini moon jae in na mwenzake wa kaskazini kim juong un walitumia gari la pamoja kukatisha katikati ya mji mkuu wa korea kaskazini Pyongyang ambapo maelfu ya raia waliojipanga barabarani waliwashangalia wakisema ‘Muungano wa taifa' na kupeperusha bendera za korea zote mbili, wakiashiria haja ya kuungana tena korea hizo mbili.
Nchini korea kusini lakini mkutano huo umeandamwa na maadamano ya wananchi wanaopinga ushirikiano wa karibu na Korea kaskazini.
Moon ambaye aliwasili Pyongyang siku ya jumanne alilakiwa kwa gwaride la kijeshi na heshima ya zulia jekundu mbele ya mwenyeji wake Kim Jong Un ambaye uwepo wake katika uwanja wa ndege umetajwa na vyombo vya habari kuwa jambo la kushangaz