Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:46 am

PICHA 3: MKUU WA WILAYA WA HAI AMEAMURU KUKAMATWA MKURUGEZI WA TUDELEY

Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa mara moja kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley, Jensen Natal na mwanasheria wa kampuni hiyo, Edward Mroso kwa tuhuma za kuikosesha serikali kodi ya zaidi ya Sh Milioni 700 kupitia kampuni hiyo.

Jana Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo aliwataka Wakuu wapya wa Wilaya kuacha kufanya kazi kwa kutaka kiki za ajabu ajabu za kuwakamata watu na kuwaweka ndani masaa 48 bila sababu ambayo amesema inaweza kupelekea watu kuichukia Serikali yao

Jafo alisema kuwa sheria zinaruhusu lakini ni pale ambapo jinai inatakiwa itendeke machoni pa Mkuu wa Wilaya, kwa kuzuia hilo jambo lisitendeke ndio Mkuu wa Wilaya anatakiwa atumie Sheria hiy

Huyu ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Jensen Natal akipelekwa kwenye karandinga baada ya kukamatwa na Jeshi la polisi

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Jensen Natal na mwanasheria wake wakiwa kwenye gari la polisi baada ya kukamatwa na Jeshi hilo.