- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
PICHA 10: ILIVYOKUWA KWENYE MAZISHI YA DADA YAKE RAIS MAGUFULI
MWILI wa Monica Magufuli, dada wa Rais John Magufuli umezikwa leo tarehe 21 Agosti mwaka huu, nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita Kabla ya mwili huo kuzikwa, ilitangulia misa takatifu ya kumuombea marehemu Monica iliyoongozwa na Baba Askofu Mkuu Mwandamizi, Yuda Thaddeus Ruwaichi.
Baada ya misa hiyo, Rais Magufuli aliwaongoza mamia ya watu waliojitokeza kumzika marehemu dada yake Monica aliyefariki dunia tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa napatwa matibabu.
Viongozi mbalimbali wa serikali na wastaafu washiriki mazishi ya marehemu Monica, wakiwemo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakati shuguli za mazishi zikiendelea katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita