Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:37 pm

NYALANDU "WABUNGE TUSIKUBALI HOJA ZINAZO LENGA KUKIUKA UKOMO WA MUDA WA UONGOZI"

Dar es salaam: Mbunge wa Singida kaskazini Lazaro S. Nyalandu ameendelea kuweka mkazo Juu ya upatikanaji wa katiba mpya, akiandika kupitia ukurasa wake wa twitter Nyalandu amesema kuwa wabunge wasikubali hoja itakayo kiuka muda wa ukomo wa madaraka

"Wabunge TUSIKUBALI hoja zinazo lenga kukiuka UKOMO wa muda wa UONGOZI uliowekwa KIKATIBA wa miaka MITANO. Tujikitike kupata KatibaMpya TZ."

Nyalandu amewashukuru wabunge wenzake kutoka vyama mbalimbali kuonesha dhamira ya kumuunga mkono juu ya hoja ya kurudishwa kwa Rasimu ya katiba mpya ile iliyoandaliwa na Jaji Warioba mwaka 2015 "NawashukuruWABUNGE wenzangu CCM na UPINZANI wanaounga MKONO hoja ya kurejea upya RASIMU ya KatibaMpya kama iliyopendekezwa na TumeYaWarioba" alisema Nyalandu


Oktoba 19 mwaka huu Nyalandu alionesha dhamira yake ya kutaka kuwasilisha kwa spika wa Bunge Job Ndugai muswada binafsi wa sheria litakaloweka shariti la kurejea upya mjadala wa katiba mpya ya Tanzania ambayo watazingatia Rasimu ya katiba ya Jaji warioba