- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:WAZIRI NDARICHAKO AWARUDISHA WANAFUNZI 682 WALIOFUTWA UDSM
Dar es salaam: Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa Agizo kuwa wanafunzi wote 682 walioondolewa katika usajili wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kurudishwa haraka chuoni hapo.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu oktoba 22 jijini Dar es Salaam baada ya kufungua mafunzo ya wahasibu yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Profesa Ndalichako amesema amesikia suala hilo mwishoni mwa wiki na tayari ameshauagiza uongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kukaa pamoja na kumaliza tofauti hizo.
“Chuo Kikuu kina nafasi 3,000 tatizo lilikuwa ni la kiufundi kutokana na wanafunzi wengi kupenda chuo hicho ,hivyo nimeomba uongozi kumaliza tatizo hilo na watoto waweze kupokelewa.
“Wengi wanapenda UDSM na tatizo lilikuwa linaweza kurekebishika na wote ni idara za serikali, TCU na UDSM hawakutakiwa kushindana na ndiyo maana nimewaagiza hadi Jumamosi wawe wamemaliza tofauti zao nafikiri hadi leo saa tisa watakuwa wameshawekana sawa,” amesema Profesa Ndalichako.