- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:WANAFUNZI WAASWA KUJIKINGA NA UKIMWI.
DODOMA: Mkuu wa chuo cha VETA Dodoma Ramadhani Mataka amewaasa wanafunzi waliohitimu mafunzo mbalimbali kujikinga na kuwakinga wengine na gonjwa hatari la ukimwi pindi wawapo mtaani.
Ameyasema hayo leo wakati wa mahafari ya 34 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini hapa.
Mataka amesema ili kufikia mafanikio ni lazima kuzingatia hali yao na kujilinda kama mitaala ilivyofafanunua.
Aidha ameiomba serikali kuwapatia wahitimu vifaa vyaa kufanyia kazi na kuwanunulia magari mapya ya kujifunzia udereva na mitambo.
Mbali na hayo amesema changamoto kubwa ni ukosefu wa mashine na vifaa vya kufundishia ,gharama za uendeshaji ni kubwa na sheria ya manunuzi ppra ikiwemo sheria ya ununuzi wa magarimapya na mitambo mipya ni matumizi mabaya y pesa ya walipa kodi.
Naye mgeni rasmi katika mahafari hayo Naibu waziri wwa nchi, sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu Anthony Mavunde ameuomba uongozi wa chuo kuandika barua kwa wizara husika ili kuweza kupata kibali cha kuingiza magari ambayo yatasaidia katika ufundishaji.
Pia Mavunde amemaliza kwa kuwataka wahitimu kutumia ujuzi walioupata katika kujiajiri na kisha kuwaajiri wengine na sio kutegemea moja kwa moja ajira kutoka serikalini.Jumla ya wanafunzi 297 wakiwemo wasichana 50 halafu wavulana 47 ndio waliohitimu mafunzo hayo katika ngazi mablimbali.