Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:45 pm

NEWS:UJUMBE WA PAPA FRANCIS JUU YA WAHAMIAJI KWENYE CHRISTMAS

Vatcan:Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewataka Wakristo bilioni 1,3 duniani kutopuuza masaibu yanayo wakumba wahamiaji "wanaofukuzwa kutoka nchi zao" na viongozi ambao wako tayari "kumwaga damu kwa watu wasio kuwa na hatia".

Kauli hiyo Papa Francis aliitoa hotuba ya kukaribisha Sikukuu ya Krismasi, huku akiwatolea wito kuwa wakarimu kwa wahamiaji.

Papa Francis, ambaye anajulikana kwa jina lake aliopewa na wazazi wake Jorge Bergoglio, mjukuu wa wahamiaji kutoka Italia, alizungumzia kuhusu hatima ya wakimbizi, miaka mitano baada ya kuchukua uongozi wa Kanisa Katoliki duniani.

"Hakuna mtu anayepaswa kuhisi kuwa hana mahali hapa duniani," alisema katika hotuba yake ya jadi ya Krismasi.hayo yanajiri wakati ambapo kumeendelea kushuhudiwa makabiliano kati ya waandamanaji wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel na kufikia siku ya Jumapili, rais wa Palestina 12 walipoteza maisha.

Uamuzi wa Marekani, umeelezwa na washirika wa Palestina kuwa, umehatarisha uwezekano wa kupatikana kwa amani kati yake na Israel.