- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:TSUNAMI YAUWA ZAIDI YA WATU 400 NCHINI INDONESIA
Watu zaidi ya 400 wamethibitishwa kufariki Dunia baada ya tsunami iliyo sababisha tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 7.5 lilopiga mji wa Indonesia
Tsunami hiyo imetokea Jana Ijumaa ambapo Upepo mkali ulivuma kutoka Palu katika kisiwa cha Sulewesi kwa mita 3.
Baada ya mshtuko wa tetemeko hilo, maelfu walizimia majumbani kwao na wengine wakielekea hospitalini ,hotelini na kwenye maduka makubwa.
Kwamujibu wa mamlaka nchini Indonesia Jitihada za uokoaji zinaendelea ingawa zimepata changamoto ya umeme kuwa umekatika.Njia kuu ya Palu imefungwa kutokana na daraja kuu kuanguka pia.
Miili mingi ilikutwa ufukweni kwa sababu ya tsunami lakini idadi yake bado haijafahamika.
Msemaji wa serikali ,Sutopo Purwo Nugroho aliiambia Reuters kuwa wakati onyo lilipotolewa hapo jana watu waliendelea na shughuli zao ufukweni na hawakuchukua tahadhari ya kukimbia mara moja hivyo wakawa miongoni mwa wahanga.
Wengine waliokoka kwa kupandia katika miti ili kukimbia upepo mkali.
Tetemeko hili lilianza kwa kutangulia kwa tetemeko lingine dogo liliuwa mtu mmoja na wengine 10 kujeruhiwa wakiwa katika soko dogo la samaki huko Donggala.
Mjini Palu,Mamia ya watu walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya tamasha lililokuwa linatarajiwa kuanza ijumaa jioni.