- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:TAARIFA YA BOT KUZIFUNGIA BANK 5 KUBWA NCHINI
Dar es Salaam: Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeamua kuzifungia benki tano za kibiashara zinazoendesha shughuli zake hapa nchini kwa mwezi mmoja kutojihusisha na ubadilishaji wa fedha za kigeni kutokana na sababu ambazo bado hazijawekwa wazi na msimamizi huyo wa mabenki.
Uwamuzi huyo unaonekana kama chombo hicho kinataka kudhibiti biashara ya utakatishaji na ubadilishaji wa fedha kiholela hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa ya BoT, benki zilizofungiwa kufanya biashara ya ubadilishaji fedha kuanzia Novemba 23 ni Barclay, Exim, UBA, ABC na Azania.
“Hatua hii imetokana na kuvunjwa kwa taratibu na kanuni, waliofungiwa walikuwa aidha wanafanya biashara kinyume na viwango vinavyowekwa au walikuwa hawawasilishi taarifa za miamala waliyokuwa wanafanya,” alisema Alexander Mwinamila ambaye ni mkurugenzi wa masoko ya fedha wa BOT.
Aliongeza kuwa hatua iliyochukuliwa inalenga kusimamia kanuni na taratibu za soko la ubadilishaji fedha za kigeni kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
Mkuu wa masoko na mawasiliano wa benki ya Exim, Stanley Kafu alisema walipewa taarifa wiki iliyopita kuwa wao ni kati ya benki zilizozuiliwa kushiriki katika soko la ubadilishaji fedha za kigeni.
“Tuliarifiwa kuwa hatua imechukuliwa dhidi yetu kwa kuwa hatukuwasilisha Benki Kuu taarifa za miamala yetu ambayo tuliifanya kupitia soko la ubadilishaji wa fedha,” alisema Kafu wakati akiongea na Gazeti la Financial Times.
Kama utakumhuka siku za hivi karibuni BoT iliyafungia maduka kadhaa jijini Arusha kwa madai kuwa yanaendesha shughuli zake kinyume na sheria zinazosimamia biashara hiyo, baada ya hapo ilitangaza kuwa huduma za ubadilishaji fedha zitapatikana katika hoteli za kitalii, benki na ofisi zao.