- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:MISRI YAPIGA MARUFUKU UUZWAJI VIZIBAO VYA NJANO
Wafanyabiashara watano wa Cairo wameliambia shirika la Habari la AFP kuwa uuzaji wa vizibao vya njano hauwezekani bila idhini kutoka mamlaka husika.
Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyabiasha, "unapotaka kuuza vizibao vya njano, unatakiwa kupewa idhini na kituo cha polisi" katika eneo unakofanyia biashara.
Kwa mujibu wa mashahidi, baadhi ya wafanyabiasaha wanauza vizibao vya njano kwa siri, huku wakisema: ficha haraka! Kuuza bidhaa hii ni hatari zaidi kuliko kuuza madawa ya kulevya."
"Maafisa wa usalama wamekuja na kutuomba tusiuzi vizibao vya njano," amesema mfanyabiashara mwengine. "Wanaogopa nchii isikumbwe na maandamano baada ya yale yanayotokea Ufaransa".
Aidha, kwa mujibu wa mmoja wa waagizaji waliohojiwa na AFP, ambaye hakutaja jina lake, amri hiyo ilitolewa kwa makampuni yanayoagiza bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi "juma lililopita" kwa kuuzia tu makampuni yanayojulikana na sio watu binafsi.
Wakati huo huo, siku ya Jumanne mahakama ya Misri iliamuru Mohamed Ramadan, mwanasheria anayejulikana kwa msimamo wake kuhusu haki za binadamu, azuiliwe kwa siku 15 kwa kosa la "tishio kwa usalama".
Mwanasheria huyo, aliyekamatwa siku ya Jumatatu kaskazini mwa Alexandria, anadaiwa kuchapisha kwenye umtandao wa Facebook ujumbe ambapo anaomba wakazi wa Alexandria, kununua vizibao vya njano, amesema mwanasheria wake Abdelrahman al-Gohary.