Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:32 am

NEWS:HATIMAE RAIS MUGABE AMEJIUZULU URAIS

Breaking News:

HARARE: Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amejiuzulu nafasi yake ya Urais ambapo dakika chache zilizopita , spika wa bung la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .

Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo cha habri cha reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.

Mapema leo muungano wa maveterani wa vita vya uhuru nchini Zimbabwe ulikuwa umetoa wito wa kufanyika maandamano dhidi ya Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo ili kumshinikiza ajiuzulu na kuachia madaraka ya nchi.

Mkuu wa Muungano wa Maveterani wa Vita nchini Zimbabwe ametaka kufanyika maandamano dhidi ya Mugabe haraka iwezekanavyo na kumshinikiza kiongozi huyo ajiuzulu.

Chris Mutsvangwa amesema leo kuwa, anawataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika maandamano ili kumshinikiza Mugabe aliyekaa madarakani kwa muda wa miaka 37 ajiuzulu na kuachia hatamu za uongozi wa nchi.

Wakati huo huo, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harare mji mkuu wa Zimbabwe wameandamana dhidi ya Mugabe aliye na miaka 93 huku wakipiga nara dhidi ya kiongozi huyo wakimtaka aondoke madarakani. Viongozi wa chuo hicho kikuu cha mjini Harare wamesema kuwa, wameakhirisha mitihani iliyotazamiwa kufanywa chuoni hapo hadi wakati mwingine. Jeshi la Zimbabwe Jumatano tarehe 15 mwezi huu lilitangaza kuwa Mugabe na familia yake wapo katika kifungo cha nyumbani na kisha kumuondoa uongozini.