- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:DC DOM AZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUPUNGUZA RIBA.
DODOMA: Taasisi za kifedha ikiwemo mabenki zimetakiwa kupunguza riba katika mikopo yao ili kuwasaidia wanyonge.
Ombi hilo limetolewa Leo na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme ambaye amesema kuwa riba katika mikopo imekuwa ni kikwazo cha kufanya mabenki yakimbiwe na wateja wao.
Mndeme ametoa kauli hiyo wakati akifungua tawi la benki ya Exim katika majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Amesema mikopo mingi inayotoewa na mabenki inakuwa na riba kubwa na jambo hilo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu lakini hakuna anayeonyesha kujali.
“Serikali ya awamu ya tano inashughulika zaidi na wanyonge, nawaombeni mliangalie jambo hilo maana riba kubwa haziwasadii watu wa takaba la chini badala yake mnawaumiza zaidi,” amesema Mndeme
Akizungumzia utendaji katika tawi hilo, aliwataka watumishi wake kutanguliza weledi na kufanya kazi kwa ushindani wa ubora huku akiwaomba Exim kuongeza matawi katika mji wa Dodoma ambao unakuwa kwa kasi kubwa.
Mkuu wa kitengo cha rasimilali watu wa Exim Fredrick Kanga alisema tawi hilo limekamilisha ndoto ya muda mrefu kwa benki hiyo katika kuhamia Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi.
Kanga alisema hilo ni tawi la 33 kwa benki hiyo ambayo imefungua matawi mengine nje ya nchi lakini akabainisha kuwa watafanya kazi kwa ushindani mkubwa wa ubora katika eneo la Udom.
“Tunatambua ziko na benki zingine, tutafanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuvutia zaidi wateja, tunatambua kuna wizara zaidi ya nane ambao ziko udom na idadi kubwa ya watumishi na wanafunzi, tumejipanga kuwahudumia,” amesema Kanga
Amesema Exim inaendelea kugawa ajira ambapo sasa imeajiri wafanyakazi 703 miongoni mwao ni 12 waliopangiwa kituo cha Dodoma na saba kati ya hao walichukuliwa Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Francisco Nzalalila amesema ujio wa benki hiyo utapunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya foleni kwa mabenki.
Profesa Nzalalila amesema Udom ina wanafunzi wengi nab ado inaendelea kupokea zaidi ikiwemo mwaka huu pekee wamepanga kupokea wanafunzi zaidi ya 10,000 hivyo huduma za mabenki ni muhimu zaidi kuweka huduma zao hapo.