Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:30 pm

NEWS:DC CHAMWINO NYAMOGA AWASHUKIA MAAFISA MAENDELEO AWATAKA KUANZISHA UTARATIBU MZURI WA UKUSANYAJI TAKWIMU JUU YA VITENDO VYA UKATILI .

DODOMA: Mkuu Wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Vumilia Nyamoga, amewataka maafisa maendeleo wa Wilaya hiyo kuweka utaratibu mzuri Wa ukusanyaji Wa takwimu juu ya vitendo vya ukatili wa kiinsia vinavyotokea, ili kufikia lengo la kutokomeza vitendo hivyo.

Akizungumza jana katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Wa kijinsia yaliyofanyika kijiji cha Buigiri Wilaya ya Chamwino mjini hapa Nyamoga alisema Maafisa wakiwa na mfumo mzuri Wa ukusanyaji Wa taarifa utasaidia kujua vitendo hivyo vimekithiri au vimepungua kwa kiasi gani.

Aidha Nyamoga amewataka watekelezaji Wa sheria kubadilika na kuongeza upatikanaji Wa haki ili kuongeza Imani kwa wananchi.

Mbali na hayo amesema Wilaya ya Chamwino vitendo vya ukeketaji,ndoa za utotoni, wanaume kutelekeza familia zako vimekithiri kwa kiasi kikubwa ni kutokana na jamii kung'ang'ania mila na desturi potofu.

"Wazazi kumshauri mtoto kujifelisha mtihani shule ili asifauli aje aolewe huo nao ni ukatili," amesema Nyamoga.

Hata hivyo amewataka wananchi wa kijiji cha Buigiri kuhamasishana na kushauriana juu ya vitendo vya ukatili Wa kijinsia.

Awali Akisoma Risala kwa niaba Ya Wanaharakati Wa Kutetea na Kupinga Ukatili wa Kijinsia Mwanaharakati Jenipher Chiute amesema tangu kuanza kwa ziara ya siku 16 za kupinga ukatili Wa kijinsia ambapo walitembelea kijiji cha Mlowa,Msanga na Chilonwa wamepata jumla ya malalamiko 86 ya ukatili kutoka kwa wananchi, miongoni mwa malalamiko hayo ni pamoja na wanawake kunyimwa haki ya kumiliki ardhi, malalamiko ya wanaume kutelekeza familia zao na ndoa za utotoni.

"Ili kutokomeza vitendo hivi ni lazima juhudi zifanyike ikiwa pamoja na kutoa Elimu kwa jamii," amesema Chiute.

Pamoja na hayo ameiomba serikali kuanzisha Mahakama ambazo zitakuwa zinashughulikia masuala ya kifamilia na serikali kuchukua hatua na kuwa kipaumbele katika kuthibiti vitendo hivi.

Akifafanua zaidi Chiute amesema changamoto zilizipo ni pamoja na ukosefu Wa rasilimali fedha kwa wananchi, umbali Wa vituo vya polisi ambavyo vinachangia wananchi kushindwa kutoa taarifa kwa wakati.

Naye msemaji Wa shirika la action aid Tanzania Joram Wimmo ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika juu ya vitendo hivyo viovu ili kutokomeza janga hilo.

Maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili Wa kijinsia yalianza rasmi mwaka 2006 ambapo kwa mwaka huu yalianza Novemba 25 kwa Dodoma yalifanyikia viwanja vya nyerere square na kilele yamefanyika katika kijiji cha Buigiri Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Funguka ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumwachi mtu salama chukua hatua.