- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZUNGU ASEMA KODI KUBWA ZAWATIMUA WAFANYABIASHARA NCHINI
Dodoma: Mbunge wa Ilala kupitia chama tawala CCM Mussa Zungu amesema wafanyabiashara wameondoka na kukimbia nchini Tanzania kwasababu ya KODI KUBWA na kukosekana kwa mazingira rafiki katika masuala ya ulipaji wa kodi na ushuru.
“Utakuta lazima watu wengi wanahamia katika bandari yenye unafuu, namuomba waziri aendelee kuchukua ushauri wa namna gani anaweza kupunguza tariff (kodi) na kodi za ‘importation’ ishuke ziwe rafiki kwa wafanyabiashara,” amesema.
Akizungumza leo bungeni Nivemba 8, 2018 wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/20 Zungu amesema bishara katika maeneo ya bandari na maeneo mengine si rafiki kwa wasafirishaji na waingizaji wa bidhaa nchini.
Amesema gharama ya kontena la futi 20 katika Bandari ya Kenya ni Dola za Kimarekani 80 ambayo wamepunguza kutoka Dola za Marekani 103.
Hata hivyo, amesema kwa Tanzania kontena lenye ukubwa huo gharama zake ni Dola za Marekani 170 ni vigumu kwa waingizaji wa bidhaa kuvutiwa kuitumia.
Amesema katika Bandari ya Dar es Salaam inayotegemewa ‘handling charge’ kwa usafirishaji ni Dola za Marekani 100 lakini Kenya ni Dola za Marekani 60.
Aidha, ameitaka Serikali kutazama gharama za kodi na kwamba wakati wanaanza kutoza VAT walianza na kiwango cha asilimia 20 lakini ikaendelea kupungua hadi kufikia 18.
Amesema uzalishaji wa vinywaji baridi umeshuka kwa sababu gharama ni kubwa na Watanzania hawawezi kumudu kununua.
Amesema ukipunguza kodi uzalishaji utakuwa mkubwa na kwamba Serikali haitapoteza kodi bali itaongeza.
Zungu amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango kutazama gharama za uingizaji wa sukari ya viwandani na kwamba wawekezaji wanalalamika hawajarudishiwa fedha walizoweka kama deposit kwa miaka mitatu.
“Sasa zimefika zaidi ya Sh45bilioni na hii ni mitaji ya wafanyabiashara na wanalipa kodi vizuri. Serikali ikitazama maeneo ya kushirikiana nayo mapato mengi ya kodi itayapata. Viwango vikubwa vya kodi tunavyoviweka vinawakimbiza wafanyabiashara,” amesema.
Amesema wafanyabiashara wengi wanakimbilia nchi nyingine na kuomba kuwa na utaratibu mzuri wa kodi ambao utawavutia wafanyabiashara wengi nchini.