Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:59 am

NEWS: ZUNGU AISHUKIA NHC KUHUSU UPANDISHAJI KODI OVYO

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amelitaka Shirika la nyumba la Taifa (NHC) kuacha tabia ya kuongeza kodi mara kwa mara kwa wananchi ambao ni wapangaji katika nyumba hizo.


Zungu amesema hayo jana Mei 30, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, baaada ya kupitishwa kwa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza kuwa wapangaji katika nyumba hizo wengi ni maskini hawana uwezo wa kulipa kodi zinazopanda kila kukicha.


“Mkurugenzi wa shirika la nyumba, maagizo ya Waziri Mkuu umeyasikia, kaa na kamati ya wapangaji, mimi shida kwangu ni nyumba ndiyo ajenda zangu za Ubunge na Waziri Mkuu amesema muachane na haya mambo ya kupandisha kodi kiholela, hawa ni watanzania hawana uwezo huo” alisema Zungu


Kwa upande mwingine mwenyekiti huyo aliipongeza Wizara hiyo kwa kuleta mabadiriko ya kiutendaji na kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi nchini.


Jana Mei 30 2018, Bunge lilikubali kupitisha makadirio ya Bajeti ya Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 73.07 imeidhinishwa