Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 12:51 pm

NEWS: ZUMA ATAKIWA NA MAHAKAMA KUJIBU TUHUMA ZA RUSHWA ZINAZO MKABILA

Pretoria: Jana Mahakama ya Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na Rais Jacob Zuma kupinga kufufuliwa kwa mashtaka ya kutafuna rushwa dhidi yake.

Zuma na marafiki zake ambao ni maafisa wakuu katika serikali walikuwa wametuhumiwa kupokea rushwa wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti ya kushika doria na silaha nyingine.

Zuma anakabiliwa na jumla ya mashtaka 783 kuhusiana na mkataba huo wa mwaka 1999 wa ununuzi wa silaha za mamilioni ya dola.

Mashtaka hayo yaliwasilishwa mwaka 2005 kwa mara ya kwanza dhidi ya Jacob Zuma lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Bw Zuma kuwania urais.

Ulipofika mwaka jana, Mahakama Kuu mjini Pretoria iliamua kwamba kiongozi huyo anafaa kujibu mashtaka hayo.

Bw Zuma baadaye aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu ya Rufaa kupinga hatua ya kufufuliwa kwa mashtaka hayo.

Rais huyo amekuwa akisisitiza kwamba hana hatia.