- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AWATAKA WANANCHI KUPAZA SAUTI KWENYE MATUKIO YA UTEKAJI
Dar es Salaam: Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama ACT-Wazalendo, na Kiongozi mkuu wa Chama Hicho Zitto Kabwe amewataka wananchi wa Kitanzania wasikae kimya na badala yake wapaze sauti yanapotokea matukio kama ya utekaji nchini Tanzania, huku akisema kuwa kukemea kunasaidia ukweli kujulikana na hata wahusika kupatikana kwa haraka.
Zitto ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 28, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Kijitonyama, Dar es Salaam.
Zitto katika mkutano wake amejikita zaidi kuzungumzia hali ya usalama nchini na mwenendo wa uchumi.
Amesema Watanzania kupaza sauti baada ya kutekwa na kupatikana kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ kumeonyesha jinsi walivyoanza kuchoshwa na vitendo hivyo.
“Haya tumekuwa tukiyasema ndani na nje ya Bunge na tutaendelea kusisitiza kwa sababu tunafahamu umuhimu wa vyombo hivi (vya Serikali). Kama wapo wachache wanaochafua taswira ya vyombo hivi ni lazima tuseme,” amesema Zitto.
“Kama vyombo hivi haviambiwi sisi ni lazima tuseme, hatua zichukuliwe kwa matukio ya awali.
Zitto amezungumzia swala la Mo aliyetekwa Alhamisi ya Octoba 11, mwaka huu katika hoteli ya Colliseum iliyopo katika mwa Jiji la Dar es salaam na kupatikana siku tisa baadae.