- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO ATAKA MALI NA MADENI YA RAIS KUTANGAZWA HADHARANI
Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe ametaka mali za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutangazwa hadharani ili wananchi wahoji kama kunatatizo juu ya mali hizo,
Akiandika kupitia ukurasa wake wa Twitter Zitto amesema kuwa imekuwa ni kawaida kwa viongozi wakubwa wa serekali kwenda kujaza fomu hizo bila kutangaza mali zao hadharani "Mmemwomba Rais aweke hilo tangazo lake wazi?'' alihoji Zitto
''Nadhani vyombo vya Habari mwende zaidi ya kuripoti ( kwa miaka zaidi ya 20 amekuwa akijaza fomu kama Waziri na baadaye Rais na pia wenzake waliomtangulia ). Twende hatua ya mbele zaidi, Mali hizi ziwekwe wazi na umma uchambue"
Jana tarehe 28 Desemba, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.
“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” alisisistiza Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.
“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.
Aidha, Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
Tamko la viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni linatolewa kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.
#Imeandikwa na Kuhaririwa na Deyssa H.Issa