- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO ASALITIWA NA WENZAKE ACT WAZALENDO
Dar es Salaam: Aliyekuwa Mwenyekiti kamati ya kampeni taifa wa ACT Wazalendo Samson Mwigamba amejivua uanachama na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM, hii imekuja Siku tatu baada ya mwenyekiti huyo kujiuzulu nyazifa zake za uenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa na ujumbe wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo,
Baada ya Mwigamba Jumatatu, Oktoba 16,2017 kuandika barua ya kujizulu uongozi na kueleza atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa ACT Wazalendo, chama hicho kilipanga kukutana Ijumaa Oktoba 20, 2017 kujadili masuala kadhaa, likiwemo la kujizulu kwake.
akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwigamba ametangaza kujivua uanachama wa ACT Wazalendo na kujiunga na CCM, amesema baada ya kutafakari kwa kina ameamua pamoja na wanachama wengine 10 kukihama chama hicho.
Amezitaja sababu za kuhamia CCM kuwa ndicho chama kinachoakisi kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo.
"Baada ya kutangaza kujivua uongozi baadhi ya viongozi wa ndani ya chama waligeuka vichaa wakinitukana kila aina ya matusi. Cha ajabu hata wale wanaofahamu na kuitetea misingi ya chama walitukanwa na viongozi wakiwepo na wamekaa kimya, hii inaonyesha wamewatuma," amesema Mwigamba.