- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AMVAA WAZIRI MAHIGA , JUU YA MGOGORO WA ISRAEL NA WAPALESTINA
Dodoma: Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Zitto Zuberi Kabwe amesema kitendo cha Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga kuonekana akigona cheasi na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kimemtia aibu taifa la Tanzania.
Zitto amesema kuwa kitendo kama hicho huenda kikaibua hisia kali kwa wananchi wa Kipalestina kwa sababu nchi hizo mbili zimekuwa na mgogoro kwa muda mrefu.
Zitto ametoa kauli hiyo leo Mei 23, 2018 katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19, nakusema Tanzania ilijenga heshima ya kupigania haki kwa wanyonge tofauti na sasa. “Tuliweka Mwenge juu ya Mlima Kilimanjaro ili umulike ndani na hata nje ya nchi na ulete upendo pasipo na upendo, matumaini pasipo matumaini, heshima palipo jaa dharau.
Ndiyo mambo yaliyopo katika sera ya mambo ya nje,”amesema. Amesema kuanzia mwaka 2016 Tanzania imeona aibu kupigia kura katika majukwaa ya kimataifa ya kuwaunga mkono wanyonge. Amesema Dk Mahiga alikuwa Israel wakati akigonganisha glasi na Netanyahu, jambo alilodai kuwa linawaumiza Wapalestina. “Nchi inaona aibu kulaani mauaji ya wanyonge walionyanganywa nchi yao. Umeonekana (Mahiga) katika televisheni ya Israel ukizungumza bila kusema lolote kuhusu wanyonge (Palestina),” amesema.