- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO ALITOLEA UFAFANUZI SWALA LA KUUZWA KWA AIRTEL
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe ameamua kulitolea ufafanuzi sakata la kuuzwa kwa mtandao wa simu maarufu nchini Tanzania la Airtel, Zitto amesema kuwa alikuwa amejizuia kulisemea jambo hili Kwa sababu mbalimbali. Sababu kubwa ni kwamba swala hii linahitaji MAARIFA kushughulikia.
Zitto asema kuwa wakati wakiwa PAC walifanyia kazi sana suala la Sera ya Ubinafsishaji. Mbunge huyo anasema kuwa Ubinafsishaji wa TTCL ni suala walilotolea Taarifa mara kadhaa Bungeni na Taarifa yao ya mwisho ilikuwa January 2015."Ni ukweli usio na mashaka kuwa Kampuni ya Celtel ( sasa Airtel ) haikulipa chochote kuwezesha kumiliki hisa kwenye Celtel Tanzania na pia uuzwaji wa Celtel kwenda Zain na kisha Airtel ulipelekea Tanzania kupoteza Mapato ya Kodi ya ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Mwaka 2011 Mzee Harry Kitilya akiwa Kamishna Mkuu wa TRA alituletea kwenye Kamati uchambuzi wa mapato tuliyopoteza ya jumla ya USD 312m kwa mauzo ya Zain kwenda Airtel. Kazi ndio iliwezesha kufanikiwa kutunga sheria ya capital gains tax mwaka 2012 na kuziba mwanya huo wa makampuni ya Kimataifa kukwepa kodi nchini kwetu." amesema Zitto
Zitto amesema kuwa jambo hili la Airtel linahitajika kushughulikiwa kwa muktadha wa zoezi zima la Ubinafsishaji nchini. Zitto anasema kuwa PAC iliwahi kumuagiza CAG kufanya Post privatization audit ya Mashirika kadhaa ikiwemo Benki ya NBC.
Pia Zitto ameligusia swala la Uuzwaji wa bank ya NBC nakusema kuwa uuzwaji wake pia ulikuwa ni wa bure na akasema kuwa huwezi kushughulika na kampuni moja moja bila kutazama muktadha mzima wa zoezi la Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.
"Ushauri wangu ni kutazama mchakato mzima wa Ubinafsishaji kwa kufanya ukaguzi maalumu wa sera nzima ili kutoa mapendekezo ya kurekebisha makosa yaliyofanyika. Hii itawezesha nchi kutoyumbayumba na matukio na badala yake kuwa na β policy consistency β kwenye jambo zima la Ubinafsishaji. Rais anaweza kuunda Tume ya Rais ( commission of inquiry) kutazama namna ubinafsishaji ulifanyika na kuchukua hatua za kisayansi baada ya matokeo ya kazi hiyo. Hili la Airtel linaweza kushughulikiwa humo na kupata matunda mazuri zaidi"
Desemba 20, 2017 Rais Magufuli alimuagiza waziri wa Fedha Dr. Philip mpango kufuatilia uhalali wa miliki ya mtandao wa Airtel kuwa kunafununu walizozipata kuwa mtandao wa simu wa Airtel ni mtandao wa shirika la mawasiliano la Taifa TTCL.