- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AKUBALI KUSHINDWA KWENYE UCHAGUZI WA MADIWANI
Dar es salaam: Kiongozi mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa wapiga kura ndio wameamua katika uchuguzi huo na wao kama chama hawanabudi kuyakubali matokeo na kujipanga katika changuzi zingine zijazo za ubunge kwenye majimbo yaliyo wazi.
"Jana tumemaliza Uchaguzi mdogo wa madiwani nchi nzima. Katika kata zote 43 nchini zilizogombewa , sisi ACT Wazalendo tuliweka wagombea kwenye kata 17 tu. Tumepata matokeo ya kata zote na hakuna kata tuliyoshinda. Wapiga kura wameamua na sisi tumekubali. Tunafanya tathmini ya matokeo nchi nzima na tutazungumza na Wananchi. Tunawashukuru sana kwa kura tulizopata". alisema Zitto Zitto amesema kuwa wao uchaguzi huu ilikuwa nikama fursa ya kuzungumza na wananchi moja kwa moja na kufikisha ujumbe kwa wananchi kutokana na kuzuiliwa kwa mikutano ya Hadhara "Hatutachoka kuendelea kusambaza sera zetu kwani tunaamini ni bora zaidi na zinazoweza kuleta unafuu kwa wananchi wetu" aliongezea ZittoZitto hakuacha kuwashukuru wananchi kwa kuchangia chama, kwani walifanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh 15 milion kama pes za kuendeshea kampeniβ Kwanza naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wote mliofanikisha kampeni hizi, kwanza wale ambao mlijitolea muda wenu , pili wale mlioitikia wito wetu wa kutuchangia fedha kwaajili ya gharama za Kampeni zetu, tukiwa tumepokea wastani wa shilingi milioni 15 mpaka sasa. Ninawashukuru sana kwa michango ya hali na mali mliyotupatia. Pia nawashukuru wananchi wote waliojitokeza kwenye kampeni zetu. Mmetufariji sana na kututia moyo kuwa inawezekana kabisa kufanya siasa za masuala ya Wananchi na kushindana kwa hoja. alisema zitto
Uchaguzi wa Maridio umefanyika jana (26.11.2017) katika kata 43 zilizopo katika mikoa 19 ya Tanzania Bara na zaidi ya vyama 4 vilishiriki katika uchaguzi huo, licha ya kutokea kwa vurugu kwa baadhi ya vituo Ambapo Kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( chadema) chenyewe kimejitoa katika uchaguzi wa kata 5 zilizopo katika wilaya ya Arumeru kutoka na madai ya ukiukwaji wa sheria, kanuni na Taratibu za uchaguzi.