Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:48 pm

NEWS: ZITTO AITAKA SEREKALI KUTOA MAELEZO KESI ZILIZOFUNGULIWA DHIDI YA JAMHURI

Dodoma: Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Zuberi Kabwe amewasilisha swali la Kimaandishi Bungeni Jijini Dodoma Leo September 4, 2018 kuitaka Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kueleza umma wa kitanzania Kuhusiana na kesi zote ambazo Jamhuri ya Muungano imefunguliwa kwenye mahakama za kimataifa za usuluhishi ya migogoro ya Biashara, uwekezaji na mikataba iliopo mjini London Nchini Uwingereza "Watanzania wanafichwa Mambo mengi muhimu" amesema Zitto

Kupitia Ukurasa wake wa Twitter Zitto amesema amechukua uamuzi huo baada ya kupitia nyaraka nyeti za kesi ya Acacia Mining dhidi ya Jamhuri ya Muungano ( LCIA Arbitration No. UN173686 no. 87 ) iliyopo London " nimegundua kuwa Serikali yetu inaficha Taarifa Kwa umma wakati Watanzania Ndio watalipa matrilioni ya shilingi"

Aidha Zitto amesema kuwa Kesi iliyoamuliwa juzi dhidi ya Shirika la Umeme la Tanzania TANESCO ilizungumzwa kwenye Taarifa ya CAG ya mwaka huu kwa Hesabu za 2016/17. "Lakini pia kesi hii haikuwa yetu kwani Benki ya SCBHK haijawahi kuwa na mkataba na nchi yetu. Uzembe mkubwa umefanyika na hivyo kubambikwa kesi si yetu" ameandika Zitto

Image result for tanesco

Zitto amemalizia kwa kusema kuwa Suala la kesi hizi za kibiashara lisipojadiliwa kwa kina watu wengine wataachiwa nchi ya kulipa madeni ya kesi tu. "Lazima tupewe Taarifa. Mf. Eco Energy Bagamoyo $500m, Symbion $600m, SCBHK $700m, Acacia $2bn! Sasa si kuuza nchi huku pengine kwa kujitakia tu? Bungeni mahala mwafaka"