- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AIBANA SEREKALI UJEZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHATO
Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto kabwe amehoji juu ya namana ulivyopatikana mchakato wa zabuni ya uwanja wa ndege wa chato ambapo ni nyumbani kwa Rais Magufuli, Akiandika kwenye ukurasa wake wa twitter Zitto ameuliza maswali kwa msemaji mkuu wa Serekali Dr. Hassan Abbas kwamba mchakato wa zabuni ya kujenga kiwanja cha ndege cha wilayani chato ulifanywa lini? na pia anataka kujua kuwa ni kina nani? walikuwa wanashindana kwenye zabuni hiyo kama inavyotaka sheria ya zabuni ya Tanzania(The Public Procurement Act, 2004)
."TZ_MsemajiMkuu ninaomba utuwekee wazi mchakato wa zabuni ya tshs 39 bilioni kwa uwanja wa ndege wa Chato. Mjenzi MAYANGA aliingia site lini? Zabuni ikatangazwa lini? Kampuni zipi ziliomba kazi hiyo? Timu ya evaluation ilikuwa na kina nani? Taarifa ya evaluation ilisema nini?" alihoji zitto
Sehemu ya Uwanja wa Ndege chato.
Mbunge John Heche akiuliza swali bungeni.
Maswali kama hayo yamewahi kuulizwa na mbunge wa Tarime mjini Heche John Heche kuhusu mchakato wa zabuni wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Chato uliopelekea kampuni ya Mayanga Contractors kupewa kazi ya tshs 39bn. Maswali ambayo Hakujibiwa. Mayanga ni Kampuni ya Nani? Imefanya kazi zipi kabla? Ilishindana na nani zabuni ya Chato Airport?Sehemu ya Uwanja wa Ndege chato ujenzi ukiendelea.