- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AGOMEA WITO WA WAZIRI LUGOLA ATAKA WITO WA POLISI
Kigoma: Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa ataripoti kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi iwapo atapata wito wa kisheria kutoka kwa polisi unaomtaka kufanya hivyo na sio wito kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.
Kauli hiyo ya zitto ameitoa Leo July 31 2018 muda mchache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola kumtaka mbunge huyo wa Act Wazalendo kuripoti Kwa kamanda wa Polisi mkoni Mtwara.
"Waziri hana hayo mamlaka. Kama polisi wananitaka watoe wito wa kisheria nitakwenda." amesema Zitto
Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT Wazalendo amesema anaendelea na kampeni za Mbunge wa Buyungu ambapo wanamuunga Mkono Mgombea wa Chadema na madiwani wa ACTwazalendo kwenye kata kadhaa. '' Nashauri Waziri ampate kwanza yule Mbwa wa Polisi Bandari" aliongeza Zitto
Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo Lugola amesema Zitto ametoa kauli za uchochezi na kuwatukana viongozi wa Serikali wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kilwa Kusini. Katika mkutano huo Zitto alialikwa na mbunge wa jimbo hilo, Seleman Bungara maarufu Bwege.