Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:41 pm

NEWS: ZITTO AAHIDI KUWASOMESHA WANAFUNZI WOTE WAJIMBO LAKE

Kigoma: Mbunge wa kigoma mjini Zitto Zuberi Kabwe amewaahidi kuwalipia ada wanafunzi wanaofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne leo 30.10.2017 ikiwa ni utaratibu wa halimashauri ya Manispaa ya kigoma ujiji iliyojiwekea kuwalipia wanafunzi wote wanaofaulu kidato cha Nne, akiwatakia kheri ya mtihani huo kupitia ukurasa wake wa facebook Zitto amewaombea dua katika mitihani yao na kusema kuwa kwa wale wanaotoka kwenye manispaa yake watasoma bure kidato cha 5 na 6

''Kwa wale wanaotoka Manispaa ya Kigoma Ujiji, mnajua mnachotakiwa ni kufaulu tu. Kidato cha Tano na cha Sita utasoma bure, manispaa yako inakulipia. Hii ndio tofauti yenu na wenzenu kutoka sehemu nyengine ya nchi yetu.

Zitto amewaahidi wanafunzi wanomaliza kidato cha sita kuwa watakutana na mpango wa ufadhili kwa elimu ya juu na kuondokana na adha za mikopo ya vyuo vikuu
''Ninyi mnaofanya mitihani Leo kutokea Kigoma, pia mtakapomaliza kidato cha sita mtakuta utekelezaji wa ufadhili wa elimu ya juu. Tunataka msimalize masomo yenu na mikopo. Utekelezaji wa Miradi yetu utakapo kamilika, mtapewa scholarship kwenda vyuo vikuu na manispaa yenu na kuondokana na adha za mikopo ambazo kaka na dada zenu wanapata Hivi sasa" alimalizia Zitto

Manaspaaa ya kigoma ujiji imekuwa na utaratibu wa kuwalipia ada wanafunzi wanao maliza kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa sere ya Taifa ya Elimu Bure na Rais Magufuli mwaka 2015/2016 kwa wanafunzi kuanzia Shule ya Msingi hadi Kidato cha nne,