- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO AACHIWA KWA DHAMANA NA KUKAMATWA TENA
Dar es salaam: Leo asubuhi Mbunge wa kigoma ujiji Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la polisi nyumbani kwake Temeke Jiji Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi cha Chang'ombe kwa mahojiano ya awali na baadaye kuhamishiwa katika kituo kikuu kanda maalum ya Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari Katibu wa Itikadi na Uwenezi Addo Shaibu amesema kuwa Zitto amehojiwa juu ya maneno aliyoyasema kwenye kampeni za udiwani katika kata ya Kijichi October 29 mwaka huu.
Ado amesema kuwa Zitto amewakilishwa na wanasheria wawili ambao ni Venance msebo na steven Mwakibolwa, Zitto alidhaminiwa na wadhamini wawili nakuruhusiwa kituoni hapo na baadae kidogo kabla hajafika mbali na kukamatwa tena.
kwa mujibu wa kamanda wa polisi kanda maalumuya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa wamemshikilia Zitto kwa kueneza lugha za uchochezi "Tunamshikilia Zitto kwa kutoa lugha zisizo na staha na kwakufanya uchochezi katika taifa, kwa sasa yupo central hapa" aliongea Mambosasa