- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZIMBABWE YAMCHAGUA RAIS WAKE BAADA YA MUGABE
Wananchi wa Zimbabwe wanapiga kura Jumatatu wiki hii kumchagua rais wao mpya baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kutimuliwa malakani mwaka uliopita baada ya kuwa madarakani kwa takriban miongo minne.
Huu ni uchaguzi wa kwanza bila kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe miongoni mwa wagombea.
Wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais ni rais wa sasa wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa ambaye anapeperusha bendera ya chama tawala cha Zanu-PF na kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa kutoka chm acha MDC.
Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa pia unafanyika sambamba Jumatatu wiki hii.
Kulingana na tafiti zilizofanywa kupitia kura za maoni Emmerson Mnangagwa, mwenye miaka 75, anapewa nafasi ya kushinda uchaguzi huo kwa kura ndogo dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa, mwenye miaka 40 , anayepeperusha bendera ya chama cha Movement for Democratic Change (MDC) katika uchaguzi huo.
Kunashuhudiwa idadi kubwa ya watu wanaopiga kura kwa mara ya kwanza nchini humo, ambako kura ya vijana ndio inayotazamwa kuwa na uzito. Takriban nusu ya watu waliosajiliwa kupiga kura wapo chini ya miaka 35.
Mamia ya waangalizi wametumwa kuhakikisha uchaguzi unakwenda sambamba, lakini mara kwa mara upinzani umetuhumu kuwepo udanganyifu katika daftari la wapiga kura.
Rais Mnangagwa, anayejulikana kama "Mamba" ameahidi kuhakikisha kuna nafasi za ajira na anaonekana kukubali kuidhinisha mageuzi ya kiuchumi.
Aliponea majaribio kadhaa ya kuuawa ambapo wafuasi wa Mugabe wanatuhumiwa kuyatekeleza