Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:48 pm

NEWS: ZAIDI YA WATUMISHI 50 WASITISHIWA MISHAHARA YAO

Watumishi wa umma zaidi ya 56 wamesimamishiwa mishahara yao kwa kile kinachodaiwa kushindwa kutoa taarifa zisizo sahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa ameagiza mishahara ya waajiri na maofisa utumishi watakaobainika kuwasilisha taarifa za kiutumishi zisizo sahihi kupitia HCMIS, itasimamishwa mara moja na Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ili kuwakumbusha waajiri na maofisa hao kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi na kwa wakati.

Wakati akisema hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Ibrahim Mahumi amethibitisha kuwa idara tayari imeshaanza kuchukua hatua kwa kuwasimamishia mishahara maofisa utumishi zaidi ya 56 walioshindwa kutekeleza wajibu wao.

Mahumi alisema watumishi wengine zaidi ya 500 wenye dhamana ya kufanya kazi kwenye mfumo wamefikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa makosa mbalimbali yanayohusu kuchezea mfumo pamoja na baadhi ya waajiri waliohusika.