Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:29 pm

NEWS: ZAIDI YA WATU 9000 MKOANI DODOMA WAPATIWA MATIBABU.

DODOMA: Zaidi ya watu 9,000 wamepatiwa matibabu katika wilaya saba za mkoa wa Dodoma huku zaidi ya watu 700 wakifanyiwa upasuaji.

Hayo yalijili baada ya jopo la madaktari bingwa wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati wakiendesha zoezi la kliniki tembezi ya kufanya uchunguzi wa afya katika wilaya ya Bahi mjini hapa.

Moja ya waganga hao akiwemo mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt James Charles amesema jumla ya sh milion 22 zilitumika katika upasuaji huku sh billion moja zilitakiwa kutolewa na wananchi wenye uhitaji wa matibabu katika wilaya zote saba za mkoani hapa.

β€˜β€™Kwa kawaida wananchi wageweza kulipia gharama ya zaidi ya sh milion 400’’,amesema.

Mbali na hayo Charles amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata huduma za afya zitolewazo na madaktari bingwa kwa lengo lakukabiliana na magonjwa yanayowasumbua.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordani Rugimbana amesema kuwa mkoa umejipanga katika kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi wote hasa waishio vijijini kwani wamekuwa wakiteseka kupata huduma za kibingwa

Baadhi ya wananchi waliopata huduma za matibabu ya kibingwa wilayani Bahi mkoani hapa akiwemo Edward Machakwaamesema wa kufuatia uwepo wa huduma hiyo umeleta manufaa kwao kwani walikuwa wakitumia muda mrefu kufuata huduma za kibingwa maeneo ya mijini