- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZAIDI YA WATU 50 WAMEFARIKA BAADA YA AJALI YA BASI KENYA
Nairobi: Taarifa kutoka nchini kenya zinasema kuwa Watu 50 wamepoteza maisha na wengine 12 kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya barabarani karibu na mji wa Kericho, Magharibi mwa Kenya.
Polisi wanasema basi la abiria linalofahamika kama Kakamega Homeboyz, lililokosa mwelekeo baada ya breki za basi hilo kukatika na kusababisha kubingiria mara kadhaa kwa basi hilo.
Kamanda wa Polisi katika eneo la Rift Valley, Zero Arome, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitalini.
“Abiria walikuwa wanasafiri kwenye Basi linaloitwa Kakamega Homeboyz, na waliojeruhiwa tumewakimbiza Hospitalini,” alisema Kamanda Arome.
Basi hilo lilikuwa limetoka jijini Nairobi kwenda mjini Kisumu na walioshuhudia wanasema, ajali hiyo ilitokea saa 11 alfajiri siku ya Jumatano.
Jackosn Koskei mmoja wa mashuhuda ameliambia Gazeti la Daily Nation kuwa, alisikia sauti za abiria wakilia baada ya mlipuko mkubwa kusikika.
Miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni watoto wanane, wote chini ya miaka mitano.
Ajali hii imetoa baada ya polisi wa trafiki kutoka ripoti inayoeleza kuwa ajali za barabarani zimeongezeka kwa asilimia nane mwaka huu nchini humo na zaidi ya watu 2,345 wamepoteza maisha.