Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 10:46 am

NEWS: ZAIDI YA WATU 190,000 INDONESIA WANAHITAJI MSAADA WA HARAKA BAADA YA TETEMEKO

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uratibu wa masuala ya kibinaadamu, OCHA limeripoti kuwa kiasi ya watu 190,000 wa Indonesia wanahitaji msaada wa dharura wa kibinaadamu kutokana na matetemeko ya ardhi na tsunami.

Ndani ya Taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo, Jumanne imeeleza kuwa idadi hiyo inawajumuisha watoto wapatao 46,000 na watu wazima 14,000, wengi wakiwa nje ya mji ambako serikali haijaelekeza sana juhudi zake za uokozi. Tangazo hilo la Umoja wa Mataifa limetolewa wakati ambapo Indonesia inapambana na shughuli za uokozi, baada ya kisiwa cha Sulawesi kukumbwa na matetemeko ya ardhi pamoja na kimbunga cha tsunami.

Msemaji wa idara ya majanga ya kitaifa na uokozi nchini Indonesia, Sutopo Nugroho anasema miundombinu mibovu inakwamisha shughuli za uokozi na kwamba mashirika ya kibinaadamu yanajaribu kuwaondoa watu katika maeneo yaliyoathirika.