Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:33 am

NEWS : ZAIDI YA WAPALESTINA 6000 WATIWA MBARONI,WATOTO NA WANAWAKE WATESWA

Zaidi ya Wapalestina 6,000 wametiwa nguvuni 2017; wanawake na watoto wanateswa kwenye jela za Israel

Zaidi ya Wapalestina 6,000 wametiwa nguvuni 2017; wanawake na watoto wanateswa kwenye jela za Israel

Kituo maalumu cha Palestina kinachoshughulikia masuala ya mateka kimetangaza kuwa zaidi ya Wapalestina elfu sita wametiwa nguvuni na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mwaka huu unaomalizika wa 2017.

Ra'fat Hamdunah, mkurugenzi wa kituo cha masuala ya mateka wa Palestina amesema, makadirio waliyofanya yanaonyesha kuwa utawala wa Kizayuni umeshadidisha wimbi la utiaji nguvuni watu, kuvamia nyumba zao na kuwafanyia upekuzi nyakati za usiku, ambapo katika mwaka huu wa 2017 askari wa utawala huo haramu wamewatia nguvuni jumla ya Wapalestina 6,400.

Hamdunah ameongeza kuwa kati ya waliotiwa nguvuni, kuna wanawake 62, vijana chipukizi 300 na wabunge 12 wa bunge la Palestina.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo kituo cha kushughulikia masuala ya mateka wa Palestina kimesema kina wasiwasi kutokana na kuendelea utesaji na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala wa Kizayuni.

Askari za Kizayuni akiwashambulia wanawake na watoto wa Kipalestina

Taarifa ambayo imetolewa na kituo hicho imeeleza kuwa hivi sasa kuna wanawake na wasichana 58 wanaoshikiliwa kwenye jela za Israel, miongoni mwao wakiwemo wasichana 10 walio chini ya umri unaokubalika kisheria na kwamba watu hao wanaishi katika hali mbaya huku wakiteswa na kuadhibiwa.

Kituo hicho kimebainisha kwamba, katika kipindi cha wiki zilizopita utawala wa Kizayuni umezidisha harakati za kuwakamata na kuwaweka kizuizini wanawake na wasichana Wapalestina, ambapo kesi ya karibuni kabisa ni ya kukamatwa A'had At-Tamimi, binti chipukizi wa Kipalestina pamoja na mama na jamaa yake kwa kosa la kukabiliana na askari wa Kizayuni.

Kwa kawaida mahakama za utawala haramu wa Israel huwa zinatoa hukumu kali za vifungo dhidi ya wanawake na wasichana wa Kipalestina