Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:40 pm

NEWS: ZAIDI YA WANAFUNZI 350,000 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KESHO

Dar es salaam: Kesho wanafunzi wa kidato cha nne wanakusudiwa funya mtihani wa Taifa, Watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kufanya mtihani huo nchini nchima.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jumapili, Oktoba 29,2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema kuwa wanafunzi 385,938 watafanya mtihani na kati ya watahiniwa hao, 323,513 ni wa shule na 62,425 ni wa kujitegemea.

Msonde amesema kuwa mtihani huo utaanza kesho saa mbili asubuhi Oktoba 30,2017 hadi Novemba 17,2017.
Dk Msonde amesema maandalizi ya mitihani yote yameshakamilika."Hivi ninavyozungumza mitihani imeshafika kwenye vituo.”

Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unafuatwa.
Katibu mtendaji huyo amewataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo.

"Mliyojifunza yanatosha fanyeni mitihani kwa kufuata utaratibu uliowekwa," amesema.
Dk Msonde amesema baraza hilo halitasita kuwafutia mitihani wote watakaojihusisha na udanganyifu.