November 27, 2024, 4:35 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZAIDI YA KAYA 62 ZIMEKOSA PAKULALA BAADA YA ZOEZI LA BOMOA BOMOA
Tabaora: Mkuu wa Idara ya Mipango miji mkoani Tabora, Asanga Mwakalukwa ameamuru kubomolewa kwa Zaidi ya nyumba 50 zilizokuwa zimejengwa katika eneo la shule ya sekondari Tabora wasichana, Nyumba hizo zimebomolewa kwa madai ya mamlaka kuwa ni wananchi wamevamia eneo la shule.
Mwakalukwa amesema kuwa ubomoaji huo umepitishwa nakubarikiwa na vikao vyote vya Manispaa ya Tabora na kwamba wakazi hao wamevamia maeneo hayo yaliyokuwa yamepimwa tangu mwaka 1958“Wavamizi hawa walipewa taarifa muda mrefu lakini walipuuzia hivyo tumeamua kubomoa ili kurudisha maeneo ya shule kwa ajili ya kufanyia shughuli nyingine za miradi,” amesema Mwakalukwa
Kwa mujibu wa Mwanasheria wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Richard Lugomela, amesema ubomoaji huo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa la Aprili mwaka huu wakati alipokuwa ziara ya kikazi ambapo aliagiza watu wote waliovamia maeneo ya shule kuondoka.Lugomola amesema eneo hilo lililokuwa limevamiwa lilikuwa na visima 11 ambavyo vingewasaidia wanafunzi kupata maji kwa karibu tofauti na ilivyosasa