Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 10:36 am

NEWS: ZAIDI YA BIASHARA 4,000 ZIMEKUFA NA ZINGINE KUFUNGWA NCHINI

Morogoro: Biashara 4,640 zimefungwa na Zingine kufa hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na vikwazo mbalimbali vikiwemo sera kandamizi zilizopo kwa sasa na mazingira magumu ya biashara nchini.


Akiongea leo Mei 17, 2018 katika kongamano la kambi ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema kinachochangia biashara nyingi kufa au kufungwa hapa nchini ni pamoja na sheria kandamizi huku akibainisha kuwa mfuko huo kwa sasa upo tayari kusaidia maeneo mbalimbali ya ujasiliamali pamoja na kutoa elimu.Godfrey Simbeye

Amesema Tanzania inatakiwa kupiga hatua zaidi katika suala ujasiriamali kwa sababu ni sekta pekee inayozalisha ajira kwa wingi nchini, hivyo ni vyema ikatumika kitaaluma katika kuwaandaa wanafunzi kufùndishwa kwa vitendo wanapokuwa vyuoni. “Sekta binafsi ni mwajiri pekee wa kudumu katika maisha ya mtu ama watu hivyo vijana wetu wanatakiwa kuwa wathubutu na kuondokana na uwoga kwani ni tatizo kubwa kwa vijana wetu,”amesema Simbeye.