Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:57 am

NEWS: WEMA SEPETU ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI, ADAIWA KUFANYIWA UPASUA

Dar es salaam: Muigizaji maarufu wa filamu nchini Wema Abraham Sepetu ameshindwa kufika mahakamani leo May 29 kwenye kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevyana kwa madai kuwa yupo Nchini India kwa matibabu.

Taarifa hiyo imetolewa na Mama mzazi wa Mwiigizaji huyo Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani ambapo wakili alishangazwa na taarifa hizo na kudai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria.

Baada ya kutoa maelezo hayo Mama Wema akatoa nyaraka za binti yake za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 13,2018.