Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:48 am

NEWS: WEMA SEPETU AFUNGIWA KWA KUSAMBAZA PICHA NA VIDEO CHAFU

Dar es salaam: Taarifa kutoka kwenye industry ya Bongo Move zinasema kuwa Bodi ya Filamu nchini Tanzania imemfungia muigizaji maarufu wa Tanzania Wema Abraham Sepetu kwa muda usiojulikana.

Akitoa uwamuzi huo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fisoo ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, Wema amewahi kuonywa lakini hajajirekebisha hata kidogo.Image result for wema sepetu

Amesema, alichofanya Wema kimelidhalilisha Taifa, kimesababisha watazamaji waige tabia, mwenendo na desturi zisizofaa na kukiuka maadili yaliyo kwenye utamaduni wa Mtanzania.

Fisoo amesema, Wema anafungiwa masuala ya filamu na uigizaji hadi bodi itakapojiridhisha kuwa amejirekebisha na itafuatilia kwa karibu mwenendo wake.

Lakini Wema jana aliiomba radhi Serikali, Bodi ya Filamu, familia, mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kutokana na kosa la kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii.

Image result for wema sepetu

Tangu wiki iliyopita kumekuwa na video chafu za faragha zinamuonyesha Wema akiwa na mwanaume zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii katika kurasa za watu mbalimbali ikiwemo ya kwake mwenyewe Wema.

Wema amewaeleza waandishi wa habari kuwa, anakiri kuwa amekosa kwa kuwadhalilisha na kuwafedhesha wengi akisema kilichotokea kimemuumiza na kumpa somo kubwa.

“Sihitaji kumlaumu yeyote, kosa ni kosa haijalishi ilikuwaje, siombi radhi kwa kutafuta huruma ya mtu yeyote bali kukiri kuwa nililofanya ni baya. Huenda ni vitendo vya kawaida au vinavyofanywa na wote lakini vinapotoka nje huwa vinaleta taswira tofauti na isiyopendaza,” amesema.

Amesema kitendo hicho ni zaidi ya aibu na kinapaswa kilaaniwe vikali na kukiri kuwa huenda anaweza asieleweke kutokana na historia ya maisha yake yaliyopita.

Wema amesema, anashukuru yaliyotokea sasa kwani tangu ameingia kwenye dunia ya umaarufu mwaka 2006 alipotwaa taji la Miss Tanzania, amegundua kuwa amefanya utoto na ujinga mwingi ambao umekuwa ukiwavunja nguvu watu waliokuwa nyuma yake hata wale wasiomuunga mkono.

“Kwa sababu labda sikuona athari ya vitu, na mimi naathirika vipi, lakini mara nyingi tunahitaji kufinywa ili uamke, nakiri nimefinywa hasa,” amesema na kuongeza kuwa tangu juzi amekuwa hayupo sawa akitafakari mwelekeo wa maisha yake akiahidi kutorudia makosa ya aina hiyo.