Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:53 am

NEWS : WEMA AMWAGIA SIFA RC MAKONDA, ASEMA ANAJIVUNIA KUWA NAE

NYOTA wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye amerejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni akitokea CHADEMA, amefunguka ya moyoni kuhusu utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.


Wema ambaye amekuwa karibu na RC Makonda tangu arejee CCM, amepost picha ya Makonda kupitia Instagram yake na kuandika ujumbe unaowataka wakazi wa Dar es Salaam kujivunia mkuu huyo kutokana na utendaji wake wa kazi.

“Tanzania Kwanza. Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi… Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa,”aliandika Wema.

Aliongeza, “Ipo siku wataelewa tu, The Man Himself… Call Him Mr Dar-es-salaam… Viva RC wangu…. Viva Rais wangu…. #UzalendoKwanza … cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be…. We support you fully,”

Muigizaji huyo bado anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya baada ya kudaiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake kupitia kampeni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanzishwa na RC Makonda.