- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA ULINZI WA MAREKANI AJIUZULU
Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis ametangaza kujiuzulu wadhifa wake baada ya kumuandikia barua Rais wa Marekani Donald Trump mapema leo.
Rais Trump ametangaza leo kwamba waziri Mattis atastaafu mwishoni mwa Februari mwaka ujao. Mattis amekuwa akichukuliwa kama mhimili wa utulivu katika baraza la Trump linalobadilikabadilika.
Uamuzi huo wa Mattis ulitarajiwa baada ya tangazo la Rais Trump la kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Syria, hatua ambayo imewakasirisha washauri wake na washirika wa Marekani.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Jim Mattis amesema anaamini kwa dhati kwamba Marekani inahitaji kuendeleza ushirikiano imara na washirika wake, na kwamba inapaswa kuweka msimamo usio na utata dhidi ya mataifa kama China na Urusi.
Jenerali huyo mstaafu pia amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mpangilio wa namna dunia inavyoongozwa, ambao amesema unasimamia vyema maslahi ya Marekani kiusalama, kiuchumi na kimaadili.