- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi wa Ufaransa Gérard Collomb hatimaye amejiuzulu wadhifa wake Hatua ambayo imewashangaza wengi nchini Ufaransa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hatimaye amekubali ombi hilo la kujiuzulu kwa waziri huyo na amemtaka Waziri Mkuu Edouard Philippe kukaimu nafasi hiyo, ikulu ya Elysée imetangaza usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii. Baraza la Mawaziri linatarajia kukutana Jumatano wiki hii ofisi ya rais imeongeza.
Uamuzi huu umewashangaza wengi, jambo ambalo halijawahi kutokea katika tangu rais Macron kuchukuwa madaraka.
Emmanuel Macron "amekubali kujiuzulu kwa Gérard Collomb na kumwomba Waziri Mkuu kukaimu nafasi hiyo kwa kusubiri uteuzi wa mrithi wake" katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ikulu ya Elyséee imetangaza mapema Jumatano wiki hii.
Mapema Jumanne jioni, uvumi - ambao ulithibitishwa usiku- kuhusu hatua ya Waziri Mkuu kufuta ziara yake iliyokuwa imepangwa wiki hii nchini Afrika Kusini ilionekana kuwa suala la Gérard Collomb lilikuwa kipaumbele kwa serikali.
Kiongozi huyo nambari 2 wa serikali aliwasilisha kwa mara nyingine barua yake ya kujiuzulu kwa rais Macron Jumanne wiki hii, chini ya saa 24 baada ya rais kukataa ombi lake la kujiuzulu, akisema kuwa bado ana imani naye.
Awali Gérard Collomb alilithibitisha gazeti la Fgaro kuwa yuko tayari kujiuzulu.
Tayari maswali mengi yameibuka kuhusu hatua hiyo ya kujiuzulu ya Gérard Collomb