- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA KILIMO AHIDI KOROSHO YOTE KUBANGULIWA NCHINI
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa wizara yake itatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho yote inabanguliwa hapa nchini.
“Baada ya kujiridhisha tumeamua sasa hahutasafirisha korosho ghafi tunataka korosho yote iwe inachakatwa nchini kwenye viwanda vyetu, kwa hiyo korosho zote zilizokuwa zinachukuliwa na wafanyabiashara kwenda kubanguliwa sijui wapi huko tumezuia” Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema kuwa viwanda vya kubangua korosho nchini vingi vimekufa kwa sababu ya ubadhilifu wa wananchi wachache na baadhi ya hujuma za watu lakini serikali imedhamiria kuanza kubangua kwenye viwanda vilivyopo kabla ya hatua za kuanzisha viwanda vingi vya ubanguaji.
“Tunamuwezesha mkulima kwa bei ya shilingi 3300 ili imsaidie kufanya kazi zake zingine ili aweze kuongeza uzalishaji katika msimu ujao wa mwaka 2018/2019 na kuepuka kushuka kwa uzalishaji” Alisisitiza Mhe Hasunga.Alisema baada ya kukamilika uhakiki wa maghala yote ya kuhifadhia korosho serikali itaanza kulipa malipo yote stahiki kwa wakulima yatakayotolewa na Benki ya kilimo Tanzania (TADB).
“Na tumeshaandaa fedha zao tunataka wakulima walipwe haraka iwezekanavyo lakini tumeanza kumjali mkulima kwanza halafu taasisi zingine zinazofaidika na korosho zitafuata” Alisisitiza