- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA KIKWETE ASHANGAZWA NA KAULI YA DK BASHIRU
Dar es salaam: Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kipindi cha awamu ya Nne Khamisi Kaghasheki ameoneshwa kushangazwa baada ya Katibu mkuu wa CCM juzi kutoa kauli kwa kusema kuwa kura za CCM zinazidi kuporomoka siku hadi siku katika chaguzi na wananchi wamekosa imani ya kupiga tena kura.
Mbunge huyo wa Bukoba mjini amesema kuwa maneno aliyoyaongea katibu mkuu wao ni yanamtizamo mpana lakini maneno kama hayo angeongea mbunge au mwana CCM kama yeye anahisi Angezongwa na asingeachwa salama na wanachama wa chama hicho.
"Nimeyaelewa vizuri sana maelezo ya Dr. Bashiru kuhusu upigaji kura wa wananchi, uhalali wa serikali, matamshi ya viongozi nk. Anao mtizamo mpana kuhusu Chama chetu na Taifa letu. Maneno yale yale ningeyasema mimi naamini baadhi ya wanachama wenzangu wasingeniacha salama" amesema Khagasheki kupitia Ukurasa wake wa Twitter
Dk Bashiru juzi October 4 alisema kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ulizalisha Serikali isiyokuwa na uhalali wa kisiasa kwa kwasababu watu wengi hawakujitokeza kupiga kura.
Huku akisema kuwa hata ushindi wa CCM unazidi kuporomoka siku hadi siku kutokana na wapigajikura kukosa imani na mifumo ya uchaguzi, ikiwa pamoja na vyama kutoa rushwa za mavazi na pesa.
"Sasa wapigaji kura wajanja wa Tanzania wameanza tabia ya kudharau uchaguzi,β alisema Dk Bashiru mbele ya wakulima waliofurika kwenye ukumbi huo.
β(Wameanza tabia) Ya kukaa nyumbani kwa sababu wanaona ni kituko, ni mchezo wa kuigiza. Ndio maana leo kupata watu kwenda kupiga kura imekuwa shida. Note (angalia), tunakoshinda ni chini ya asilimia 30, chini ya asilimia 40. Hakuna mahali ambako wapigajikura wamejitokeza kwa asilimia 50," alisema Dk Bashiru.
Kauli ya Khagheki inaonesha kuwa wapo watu ndani ya CCM wanao uwezo wa kusema chochote na hakuna mtu wa kumzongazonga na wako wanachama wengine wakizungumza maneno ya kutaka kukikosoa chama hicho wanaonekana kana kwamba wanaunga mkono upande wa vyama pinzani.