- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI UMMY ''ZOEZI HILI SIYO GENI LILIANZA TOKEA MWAKA 2015''
DOM: Serikali imesema imekuwa ikitoa kingatiba kwa wanafunzi wenye umri wa miaka mitano hadi 14 na sio chanjo ili kuwakinga watoto hao dhidi ya ugonjwa wa kichocho na minyoo tumbo.
Kauli hiyo ya serikali inajibu taarifa iliyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya zoezi hilo kufanyika katika Jiji la Dar Es Salaam kuonekana kupata maudhi kwa baadhi ya watoto kama kupata kizunguzungu.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi juu ya kinga hiyo ya vidonge ambayo imekuwa ikitolewa kwa watoto hao hususan mashuleni.
Waziri Ummy amesema zoezi hilo sio geni lilianza tangu mwaka 2015 katika halmashauri zilizokuwa na maambukizi mengi lakini kwa sasa linafanyika kwa halamshauri zote na kuweka bayana mafanikio yaliyopatikana.
Wakati huo huo waziri Ummy amewatakia kheri watoto wa darasa la saba walioanza mtihani wao hii leo huku akisisitiza wajibu wa wazazi na walezi kuweka mazingira wezeshi ya mtoto kuendelea na elimu ya sekondari.