- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI UMMY AWASHUKIA WANAOTUMIA JINA LAKE KUTAPELI WATU.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amekanusha vikali kuhusika na tangazo na umiliki wa ukurasa wa mtandao wa Facebook wenye chapisho la matapeli wa mtandaoni linalotangaza ajira za Shirika la Msalaba Mwekundu kwa watu 100 kila wilaya nchi nzima lilioandikwa TANZANIA RED CROSS JOB APPLICATION FORM.
Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika: “Huu ni UTAPELI, Sihusiki na Sijui lolote kuhusu Kazi za Red Cross, na nimewaomba TCRA kufuatilia na kuwachukulia hatua wahusika/matapeli hawa.”
Katika tangazo hilo, muombaji wa ajira anatakiwa kutuma pesa kiasi cha Tsh. 10,000/= wanazodai kuwa ni za uanachama na kuzituma kupitia M-pesa namba 0767291550 (yenye jina la Mr. Shabu Lifumike, Ofisa Muajiri Mkuu).