- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUKA SABABU ZA KUPOTEA KWA UZALENDO WA TAIFA.
DOM: Mmonyoko mkubwa wa maadili nchini ni miongoni mwa sababu inayopelekea Watanzania wengi kushindwa kuenzi uzalendo wa Taifa lao.
Akifungua mtahalo wa kumbukizi ya hayati mwalimu Julius Kambarange Nyerere uliofanyika katika chuo cha Mtakatifu Yohana jana jijini Dodoma Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe alisema maisha aliyoyaacha Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere yamebadilika sana hii ni kutokana na utandawazi watu wamekuwa wakijifunza vitu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii nahii hupelekea kushindwa kuthamini vya kwako na kuiga vya nchi nyingine ikiwemo mavazi.
"Kipindi alichotuacha nacho Mwalimu Nyerere si kilekile saivi kimebadilika sana ni kutokana na utandawazi na maendeleo ya kasi sana ya teknolojia ya habari na mawasiliano vitu ambavyo vimeleta maendeleo makubwa lakini vilevile vimeleta athari kubwa hasa katika nchi zetu zinazoendelea"amesema Waziri Mwakyembe.
Pia"Kuna mmonyoko wa kasi kubwa kweli kweli wa maadili yetu ikiwemo suala la mavazi yasiyokuwa na staha, Matendo na matamshi yasiyostahili kwa watoto na wazee hatuwalaumu watoto tu hata wazee watu wazima kuropokaropoka tu vitu vya ajabu ajabu vilikuwa ni vitu ambavyo haviko kwenye maadili ya mtanzania" ameongeza kwa kusema .
Amesema ulimbukeni uliopitiliza watu wanathamini sana vya kigeni kuliko vya kwao na kuongea kuwa watu wanathamini lugha ya kigereza ambacho kilitumika kuwatawala kuliko kiswahili ambacho kilitumika kuwapatia uhuru ,kiswahili ni lugha inayotumika kutambulisha Taifa letu na iliyotumika katika ukombozi wetu.
Akiwalisha mada katika mdahalo huo isemayo"Maisha na uongozi wa hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarange Nyerere yanavyoakisi Uzalendo na Utaifa" Kaimu Mkuu wa idara ya Taaluma za Rushwa kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana Dkt Alfred Sebahene amewataka viongozi na watanzania kuyaishi maisha ya mwalimu Nyerere ikiwemo utawala bora na kuishi maisha yenye uhalisia.
Akinuku maneno ya Mwalimu Nyerere Kaimu wa chuo cha Mtakatifu Yohana Dkt sebahene alisema ‘’Madhari nia niliyonayo ni nzuri basi sitageuka nyuma na kuwa jiwe, Ikulu ni mahali patakatifu anayekimbilia ikulu ni wakuogopwa kama ukoma CCM si mama yangu ikiacha misingi yake nami naicha kaburu ni kaburu tu si lazima awena na ngozi nyeupe.’’
Akiendelea kufafanua amesema maudhui ya nukuu hizi inakupa picha halisi ya kutafakarishwa uhalisia wa maisha na uongozi wa Mwalimu na kuongeza kuwa pia inakupa uhalisi wa maisha ya Mwalimu katika utawala wake pindi akiwa hai.
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa moja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini, Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu ( leukemia).