Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:46 am

NEWS: WAZIRI MPINA ATAIFISHA TANI 65 ZA SAMAKI

Kagera: WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina ametaifisha zaidi ya tani 65.6 za samaki aina ya Kayabo wenye thamani ya Sh milioni 300 waliovuliwa kinyume cha sheria katika Kisiwa cha Rubili kilichopo wilayani Muleba mkoani Kagera wakiwa tayari kutoroshwa kwenda nchi za Rwanda na Uganda.

Mpina ametoa maamuzi wa samaki hao wauzwe kwa mnada wa hadhara huku akisisitiza kuwa, wafanyabiashara wenye leseni halali za kusafirisha mazao ya uvuvi nje ya nchi ndio watakaopewa kipaumbele katika mnada huo. Akizungumza mjini Bukoba walikohifadhiwa samaki hao jana, Waziri Mpina alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dk Yohana Budeb, kuwapa wiki mbili wenye leseni za usafirishaji wa samaki na mazao yake kuhuisha leseni zao kwa kuwaongezea masharti mapya.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuambatanisha taarifa zao za ulipaji kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusisitiza kuwa, watakaoshindwa kukidhi masharti hayo mapya, wafutiwe leseni zao na wasiruhusiwa kujihusisha na biashara hiyo. Alisema samaki hao wachanga na wazazi waliovuliwa chini ya sentimita 30 na zaidi ya sentimita 85 wamekatishwa maisha yao.