Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:06 pm

NEWS: WAZIRI MKUU WA UBELGIJI AJIUZULU

Waziri mkuu wa Serekali ya Ubelgiji Bw. Charles Michel ametangaza kujiuzulu kufuatia Hasira ya wazalendo juu ya mvutano kuhusu uhamiaji nchini humo

Hatua hiyo imekuja Ikiwa imesalia miezi mitano tu kabla ya kufanyika uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Mei haikuweza kubainika ikiwa mfalme Philippe angeridhia uamuzi wa ghalfa wa Michel.

Taarifa ya ikulu imesema bado uamuzi unasubiriwa ingawa chanzo kimoja kimesema huenda utawala wa kifalme utaitaka serikali ya Michel kusimamia shughuli za kila siku za serikali hadi pale kalenda ya uchaguzi itakapo tajwa.

Siku ya Jumapili katika mjadala wa bungeni, waziri mkuu huyo, Mliberali alikitri kushindwa kukabiliana na kura ya kutokuwa na imani ambayo iliitishwa na vyama vya mrengo wa kushoto na upinzani.

Michel, ambaye aliingia madarakani mnamo 2014 alipoteza uungwaji mkono na chama chake (N-VA) kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa wa uhamiaji.